Wanyakyusa huwa
tunaita (Nsighwana) yaani mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa. Huyu mtoto ana nguvu sana katika ulimwengu wa
roho na mpaka kwenye ulimwengu wa kimwili, na hizo nguvu zimegawanyika kwenye
maeneo mawili:
1) Eneo
la Kwanza, huyu mtoto huwa anafanyika kama
lango la baraka.
Haijalishi
anaishi mazingira gani, au anaishi na walezi ambao siyo mama yake wa kumzaa au
baba yake wa kumzaa, pengine anaishi na bibi yake au amepanga. Lakini muda
mwingine huyu mtoto, Mungu huwa anamtumia kama
lango la baraka.
“Basi
huyo Yefta, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa
mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yefta. Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na
hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekuwa wakubwa wakamtoa Yefta, na kumwambia,
Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke
mwingine. Ndipo Yefta akawakimbia hao nduguze, akakaa katika nchi ya
Tobu;……….wakaenda kumtwaa huyo Yefta katika ile nchi ya Tobu; wakamwambia
Yefta, Njoo wewe uwe kichwa chetu, ili tupate kupigana na wana wa Amoni”
(Waamuzi
11:1,3;5,6)
Huyu Yefta,
alikuwa ni mtoto wa nje ya ndoa lakini Mungu aliachilia nguvu zake na baraka
juu yake kwa ajili ya familia yake na kwa taifa zima la Israeli. Nimeona
watoto, vijana wengi wanakuwa na akili sana
darasani lakini ukifuatilia vizuri mmoja wapo, kuishi kwake na wazazi wake,
utashangaa akikwambia anaishi na mama tu! kwani alitelekezwa na baba, na kwenda
kuoa mwanamke mwingine. Wengine wanamaisha mazuri, Mungu kawabariki lakini baba
alimkataa, na huko baba yake aliko maisha yake yanakuwa siyo mazuri sana. Ni wakina baba
wangapi wamezaa nje ya ndoa na wamewakataa hao watoto, na maisha yao hao wazazi yakoje?
Kama siyo mlevi basi atakuwa ni Malaya, ama
mwizi. Mara nyingi kufanikiwa kwa hao watu ni vigumu sana, au anaweza kufanikiwa lakini nje ya
njia za Mungu, kitu tunachosema ni mafanikio feki na yasiyokuwa na uzima wa
milele ndani yake.
Unamkumbuka Sulemani? Fuatilia kuzaliwa
kwake ilivyokuwa. 2Samweli 12,13 (soma sura hizo). Utaona mfamle
Daudi alipokuwa akitembea juua ya dari ya jumba lake la kifalme, ghafula
akamwona mwanamke akioga na huyo mwanamke alikuwa anaitwa Bath-sheba, na
alikuwa ni mke wa Uria aliyekuwa ni askari wa mfalme Daudi. Mfalme Daudi
akafanya namna alivyofanya akampata yule mwanamke, akazini naye na yule
mwanamke akapata mimba. Mtoto alipozaliwa, Mungu akamuua yule mtoto ingawa
Daudi alifunga siku saba na kuomba sana.
Lakini yale maombi yalikuwa yanazaa tunda ambalo Mungu alilikusudia.
v
Mungu alikuwa anamwondolea aibu mfalme Daudi kwa
watu kupitia yule mtoto, endapo angeishi. Ndiyo maana mtoto alipofariki tu,
Daudi akainuka na akaacha kuomba juu ya huyo mtoto.
v
Kupitia yale maombi, Mungu alikuwa anaumba mtoto
mwingine atakaye mpenda, ambaye alikuja kuwa Suleimani, aliyezaliwa kupitia
tumbo la huyo Bath-sheba. Ndiyo maana hata Adamu ilimgharimu sana kwa muda kuja kumzaa Sethi, ambaye
atakubalika na Mungu.
Nilikuwa
namuuliza Mungu, kwanini hakutokea mtoto uliyempenda kutoka kwa mfalme Daudi,
aliyezaliwa mbali na tumbo la Bath-sheba? Nisikilize mzazi itakusaidia sana! Mfalme Daudi
alipokuwa anazini na Bath-sheba, ujue kwamba alikuwa na wake wengine nyumbani
kwake. kilichomfanya aende nje ya ndoa ni nini? Maandiko yanasema “naye huyo
mwanamke alikuwa mzuri sana,
wa kupendeza macho”. Inaonekana Daudi wake zake hakuwapenda kwa dhati kama huyu Bath-sheba. Mungu aliachlia mbegu iliyobora
kwenye tumbo la Bath-sheba kutoka kwa Daudi kwani ulikuwepo upendo wa dhati.
Unapompenda mke wako kwa dhati, ujue hata utakachokizaa kitapendwa na Mungu
kwani Mungu mwenyewe ni pendo (1Yohana 4:8), hivyo unapoingia kwenye ile
ibada na mkeo/mumeo msipokuwa na upendo wa dhati au mmekorofishana, au mnaingia
ile basi tu! Nawaambieni mtazaa mtoto mwenye hasira, muda mwingine utashangaa
anazaliwa mtoto kilema, kwa sababu mlimtafuta huyo mtoto mkiwa hamna amani wala
hamkupendana kwa dhati.
Sulemani alikuja kutumika kama
mlango wa baraka ndani ya familia ya Daudi, kwani ndiye aliyekuja kukubaliwa na
Mungu akae kwenye kiti cha ufalme alipotoka baba yake Daudi. Lakini kuzaliwa
kwake kulikuwa ni kwa hali ambayo haikuwa halali, kwani alikuwa amezaliwa nje
ya ndoa ambayo Mungu alikuwa amempatia mfalme Daudi. Fuatilia watu ambao ni
viongozi mahali mbali mbali, utaona kwamba wengine walilelewa na mama tu, kwani
baba alimkataa.
Usije ukajaribu wewe mama kumtupa mtoto
uliyezalishwa nje ya ndoa hata kama
amekutelekeza huyo mwanamume aliyekupa ujauzito. Kumbuka Hajiri:
“Akaenda
akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema,
Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka
mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya
kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa”
(Mwanzo
21:16,18)
Nataka uone neno
hili “…Mungu akasikia sauti ya kijana..” kwa nini Mungu hakusikia sauti
ya Hajiri? Mungu anapokupa mtoto kwenye wakati mgumu, haijalishi umekataliwa au
la! Lakini ujue kwamba Mungu anakuwa na makusudi na huyo mtoto, la sivyo
angeamua kumuua mapema, kama mtoto wa Daudi.
Maisha ya baraka na mafanikio ya wazazi yanafichwa ndani ya mtoto na ndiyo
maana Mungu alisikia kilio cha kijana (mtoto) ambaye alikuwa ni Ishimaili.
Umewahi kufikiria, ingekuwaje endapo Hajiri angeamua kutokwenda kumchukua
mwanae! Ni wasichana wangapi wametupa watoto, wametoa mimba, na wamekwama
kimaisha na kiroho kwani Mungu alikuwa ameachilia baraka zao kupitia wale
watoto waliowatupa.
Wazazi huwa wanaelewa, mara nyingi
inapotokea mtu kajifungua, huwa wanaelewa kuwa huyu mtoto amekuja na baraka
fulani. Utashangaa wageni wanakuwa wengi nyumbani, chakula hakiishi ndani, na
kadhalika. Wengine wanasema mtoto mchanga huwa anawaombea wazazi kwa Mungu
kwani ni malaika, ni kweli kabisa. Mungu atamsikiliza mtoto kuliko mama au
baba, na ndiyo maana Mungu alisikia kilio cha Ishamaili na siyo cha Hajiri.
Kama ulizaa nje ya ndoa, na mtoto huyo
yupo, nakushauri ukamchukue na kama
hukumwambia mkeo au mumeo, ni wakati wa kumwomba Mungu akupe ujasiri na hekima
ya kusema naye ili akuelewe na usivunje ndoa yako. Utashangaa umekwama
kiuchumi, kumbe kuna damu inakulilia huko nje. Na uwe na uhakika huyo mtoto
Mungu atakuja kumfanikisha tu, hata kama
hutamchukua, na baadaye utajutia kwanini hukuwa muwazi. Unakataa mtoto, tambua
unakataa baraka za Mungu.
2)
Usipojua namna ya kumkabidhi Mungu, huyu mtoto
anafanyika kuwa laana kwenye ndoa.
“Gidion
alikuwa na wana sabini waliozawa na mwili wake; kwa maana alikuwa na wake
wengi. Na suria yake aliyekuwako Shekemu, yeye naye alimzalia mwana, naye
akamwita jina lake
Abimeleki.”
(Waamuzi
8:30-31)
“Kisha
akaenda (Abimeleki) nyumbani kwa babaye huko Ofra, akawaua nduguze, hao wana wa
Yerubaali, watu sabini akawaua juu ya jiwe moja;…”
(Waamuzi
9:5)
Abimeleki
alizaliwa na Suria (Girl friend) wa Gidion, inamaana alizaliwa nje ya ndoa,
lakini amekuwa mwiba kwa uzao wote wa Gidion ambao walikuwa ndani ya ndoa.
Akapelekea kuwaua nduguze, watoto wa babaye Gidion.
Nimeona ndoa nyingi sana zinavunjika kwa
sababu ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa. Zingine ni ndoa za wapendwa
(waliookoka) lakini kwa kutokujua, walijikuta wakati wa ujana wao walicheza na
dunia mwishowe wakazaa na watoto. Nataka ujue sababu hasa, kwanini watoto wa
nje ya ndoa, wanapoingia kwenye mazingira ya ndoa halisi huwa wanasababisha
migogoro ndani ya ndoa. Haijalishi amebadilika ukubwani, lakini kwanini ilete
kutokuelewana kwa wanandoa na familia nzima, mara nyingine inapelekea ukoo
mzima kutokuelewana na huyo muhusika (aliyezalisha).
v
Tambua yule mtoto alizaliwa chini ya agano.
“Tena
mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na
kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu
na kuiridhia. Lakini ninyi mwasema, ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA
amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtendea mambo ya hiana,
angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako”
(Malaki
2:13,14)
Agano ni
makubaliano, mkataba, kiapo baina ya pande mbili au watu wawili. Sasa agano ambalo linanguvu zaidi ni agano la
damu, na kama ilipelekea mpaka kuzaa mtoto na
huyo msichana, ina maana agano lililotendeka hapo ni agano la damu. Kama
mlifanya uasherati inamana Mungu hakuwepo kwenye hilo agano, inamaana Shetani ndiye
aliyehusika, maana hakuwa mke wako halali mbele za Mungu. Pindi unapomwacha uwe
na uhakika lile agano linaendelea kukutafuta wewe uliyefunga na huyo
msichana/mwanamume.
Agano likitendeka la damu, mara nyingi
huwa linakuwa linahitaji damu nyingine, na ndiyo mana kama
imetokea ajali mahali fulani na ikaua watu, utashangaa ajali nyingine inatokea,
kwani kuna mapepo yanayoendelea kufwatilia damu nyingine mahali pale. Hivyo
anapotokea mtoto uliyemzaa nje ya ndoa, inamana anakuja na roho ya lile agano,
likikutaka uende tena kufunga agano lingine, yaani ukaendelee kuzini, ndiyo
maana inatokea hali ya kumchukia mke wako na kwenda nje ya ndoa tena, pasipo
mwenyewe kujua.
v Roho
ya uasherati inakuwa inafwatilia kulipiza kisasi.
Baada ya
kumwagika damu ya Habili, maandiko yanasema “….sauti ya damu ya ndugu
yako inanililia kutoka kwenye ardhi” (Mwanzo 4:10b). damu ya Habili
ilikuwa inalia ili kulipiza kisasi kwa Kaini. Hiyo damu inapokuja na kutaka
kulipiza kisasi ndani ya nyumba, inakuwa inamuhitaji mtu aliye dhaifu kati yenu
ninyi wana ndoa, ili aende kinyume na kiapo (agano) walichokifunga pale
walipokuwa wanafunga ndoa. Utashangaa sana
mke wa mtu anaamua kutoka nje ya ndoa na kuzini ilimradi amkomoe mume wake,
kwani amemwona akiwa na wengine huko, na aliwahi kuzaa nje ya ndoa. Kitendo cha
mwanamke kutoka nje ya ndoa, tayari hiyo ni roho ya kisasi inayotokana na agano
alilolitenda mume wake, kwa kuzaa nje ya ndoa.
“BWANA
asema hivi, Angalia nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa
wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako
mbele ya jua hili”
(2Samweli
12:11)
“Basi
wakamtandikia Absalomu hema juu ya nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa
masuria ya babaye machoni pa Israeli wote”
(2Samweli
16:22)
Ni habari za
mfalme Daudi, baada ya kutembea na Bath-sheba na kumpa mimba, ingawa mtoto
alikufa baada ya siku saba, na alikuwa ni mke wa mtu (Uria) aliyekuwa ni askari
wake Daudi. Yaani Daudi katembea na mke wa mtumishi wake, na akasababisha
mimba, na Mungu akamwambia Daudi kwamba na yeye atafanyiwa kama
vile vile alivyomfanyia mtumishi wake, tena pasipo siri.
v Inafuatilia
watoto.
Kumbuka
Absalomu alikuwa mtoto wa Daudi, na ndiye aliyetembea na masuria wa baba yake,
na si mtu mwingine! (1Samweli 16:22). Chunguza, kama
baba aliwahi kuzaa nje ya ndoa, utashangaa mtoto pia anakuja kuzaa nje ya ndoa.
Kama baba anazini na watoto wa marafiki zako,
uwe na uhakika, watoto wake watapewa mimba na rafiki zake hao hao. Haya mambo
yapo kwenye jamii tunazoishi nazo sisi wenyewe na siyo kuzimu! Ndiyo maana kila
siku kizazi kinaendelea kuharibika, na kufikia mpaka miaka ya kuishi inapungua
(life expand). Mtoto wa miaka kumi na mbili anazaa mtoto, yaani mtoto anazaa
mtoto.
v Inakuja
na roho ya mauti.
Kuna habari
nilisikia mkoa fulani, baba wa kambo alimuua mtoto kikatili sana, kwa wivu aliokuwa nao. Alimwoa mwanamke
ambaye alikuwa ameshazalishwa na mtu mwingine, lakini kumbe ndani yake yule
mwanamume alikuwa anamchukia yule mtoto, hatimaye ikapelekea kifo na yeye
akaishia jela. Mungu atusaidie wazazi!
v Inafunga
milango ya baraka na mafanikio.
Kunakitu ndani
ya familia yako lazima kitakwama tu! Mfano, utakuta familia zingine ni ngumu
kupata watoto kiurahisi, kama kuna mifugo, utashangaa inaanza kudhoofika mpaka
kufa, chuki kwa mke/mume wako pasipo sababu, kama
unawatoto wengine, utashangaa wanabadilika akili darasani (kushuka kwa
ufahamu). Mpaka unakuja kufikia wakati mtakapogundua kwamba chanzo ni huyo
mtoto wa nje ya ndoa, mtaanza kusema ni mchawi na kumbe siyo mchawi bali ni
roho iliyo ndani yake ambayo hata yeye anashindwa kuitambua.
Ø
Utaepukaje kama uliisha zaa nje ya ndoa?
Kaa vizuri na Mungu, uvunje hiyo roho ya uasherati.
“Basi
mtiini Mungu, Mpingeni Shetani naye atawakimbia”
(Yakobo
4:7)
Kumbuka
kuomba toba juu yako, juu ya mwanamke uliyemzalisha, juu ya mtoto husika,
pamoja na familia yako. Kuna dada mmoja, nilikuwa namfanyia maombi na shida
yake kubwa ilikuwa ni ndoa haina amani, ghafla Roho Mtakatifu akaniambia juu ya
mume wake kwamba ana mtoto nje ya ndoa. Naye akakiri kwamba ni kweli na amewahi
kumshirikisha kwamba yupo kwa ndugu zake. Na mume wake alikuwa hatulii
nyumbani, na alikuwa ana wanawake wa nje wengi sana, lakini kumbe chanzo cha magomvi yote ni
yule mtoto. Tulipoingia kwenye maombi, Mungu akanipa maelekezo ya kumrudisha
mtoto nyumbani ili akae na yule dada iwe familia moja.
Unapomleta nyumbani kama
familia moja, unakuwa unavunja nguvu ya ile roho ya uasherati, isiwe na nguvu,
ila hakikisha umekaa vizuri na Mungu, maana utajikuta unaongeza tatizo badala
ya kuondoa tatizo. Ashukuriwe Yesu Kristo yule mama akarudisha mahusiano mazuri
kwa mume wake na familia nzima.
Ø Vunja
hilo agano kwa
njia ya sadaka.
Kama agano lilitengenezwa kwa damu, ambayo damu ilikuwa
inahusika kwenye utoaji wa sadaka. Hivyo chukua sadaka na maombi yako, nenda
ukavunje hilo agano madhabahuni pa BWANA, na
Mungu atasimama kwenye hilo
eneo daima. Mungu alisema na huyo dada aliyekuwa anashida ya ndoa,
iliyosababishwa na mtoto wa nje ya ndoa kwamba atoe sadaka. Alipotoa sadaka na
nilipoanza kuiombea, ghafula nguvu za Mungu zilishuka na kumwangusha chini.
Mara pepo likaanza kupiga kelele na kulalamika kwanini ametoa sadaka, kwani
pepo linasema lilifunga agano na mume wake, na hilo agano ndilo lile la mtoto wa nje ya ndoa
pamoja na wanawake aliokuwa akizini nao. Nakumbuka ulikuwa ugomvi mkubwa sana na ashukuriwe Yesu
Kristo sadaka haikurudishwa na akafunguliwa, na ndoa yake ikaponywa.
Barikiwa sana, kwa msaada zaidi
ingia kurasa ya mawasiliano.