SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI YAKO YASIJIBIWE

Maombi, kwanza kabisa hudhihirisha uhusiano uliopo kati ya muombaji na Mungu wake-Baba, Mwana (Yesu Kristo), na Roho Mtakatifu.
      Ina maana udhihirisho wa mahusiano yenu kwamba ni mazuri ni pale tu unapokuwa unapokea na kujibiwa katika lile uliombalo.
Tukiangalia moja ya waombaji kama Yesu mwenyewe, Daniel, Habakuki, Eliya, Nehemia, n.k.
Wengi maombi yao yalifanikiwa kwa kiwango cha juu, na wengine kupewa maelekezo namna ya kuomba kama Habakuki

BAADHI YA SABABU ZINAZOWEZA KUFANYA MOMBI YAKO YASIJIBIWE.

1. Dhambi katika maisha yako.
(Zaburi 66:18; Isaya 59:1-2; Yohana 9:31)
"Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia" (Zaburi 66:18)
"Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia, lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia" (Isaya 59:1-2)
"Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu na kufanya mapenzi yake humsikia huyo." (Yoh 9:31)

2. Kujihusisha na Ibada za Sanamu, Mizimu, na miungu.
(Ezekiel 14:2)
"Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki (Haki) yangu niulizwe na wao katika neno lolote?"

3. Uchoyo (Ubahili) na Tamaa mbaya
(Mith 21:13, Zakari 7:13, 1Tim 6:10)
"Azibaye masikio yake asisikie kilio cha masikini yeye naye atalia, lakini hatasikiwa" (Mithali 21:13)
"Ikawa kwa sababu alilia, wao wasitake kusikiliza; basi wao nao watalia, wala mimi sitasikiliza, asema Bwana wa majeshi" (Zakari 7:13)
"Maana shina  moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma na maumivu mengi" (1Timo 6:10)

4. Kutokuamini na Mashaka (Yoh 16:9; yakobo 1:6-8)
"Naye akiisha kuja, atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi......kwa sababu hawaniamini mimi" (Yoh 16:9)
"Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; kwa maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari iliyochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku. maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote" (Yakobo 1:6-8)

5. Kutokusamehe na uchungu (Mathayo 6:14-15)
"Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu"

6. Jinsi Mume anvyoishi na Mke (1 Petro 3:7)
"kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja na neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe"

7. Kiburi na majivuno (Yakobo 4:3)
 "Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu"

8. Nia ya uchoyo katika maombi
  "Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu"

9. Roho yenye kuhukumu (Mathayo 7:1, Rumi 14:10)
"Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi" (Mathayo 7:1)
"Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako! Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sotetutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu" rum 14:10)

10. Kukosa shukurani (1Thes 5:18)
"Shukuruni kwa kila jambo, kwa maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo yesu"

11. Kutokutengeneza (Walawi 16:4-5)
"Mtu huyo anapokuwa ametenda dhambi na amekuwa na hatia ni lazima arudishe alichoiba au alichopata kwa dhuluma, au amana aliyopewa, au kitu cha jirani yake kilichopotea akakipata au chochote alichoapa kwa uongo. Atalipa kila kitu kikamilifu na kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Mara atakapojua kosa lake atamrudishia mwenyewe'

12. Kuupenda ulimwengu na anasa za dunia (1 Yoh 2:15)
"Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake"

13. Kutokuomba katika jina la Yesu (Yohana 14:14, Matendo 19:13)
Yaani kutokuwa na mamlaka (haki, kwa kutegemeana mahusiano yako na Mungu) ya kulitumia jina la yesu.
"Mkiomba neno lolote kwa jina langu, nitafanya"

14. Kutokuomba kulingana na mapenzi ya Mungu (1Yoh 5:14, Habakuki 2:1-3)
"Na huu ndiyo ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake atusikia"

0712-201073


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni