Mwanzo 3:1-13
1. KUTOSHIRIKIANAMazingira yaliyokuwepo kwa Hawa ndiyo yaliyompatia nafasi Nyoka (Shetani) aweze kumjaribu Hawa, kwa sababu Adamu hakuwepo katika mazingira ya tukio ndiyo maana majibizano yalikuwa ya Hawa na Nyoka peke yao na Adamu anakuja kushirikishwa baadaye.
Wanandoa wengi huwa wanajikuta wapo kwenye wakati mgumu sana kwa sababu ya maamuzi ya mmoja wao yamefanyika bila kushirikishana kwa pamoja.
Mfano: Ukatumia pesa kununulia kitu amabacho mmoja wenu hajaridhia vinapelekea ugomvi katika ndoa, au mmoja akajenga nyumba, kununua uwanja au gari au chochote pasipo kushurikishana, hicho kitu kitaleta ugomvi mkubwa sana. kunamwingine amefungua akaunti benki mbili mbili lakini mke wake au mume wake hajui, Kama wewe ni Mkristo kweli na ndoa yako inahofu ya Mungu tafadhari sana unafanya kosa, ninyi ni mwili mmoja, biblia inasema ukimpenda mke wako sawa na kuupenda mwili wako, hivyo ukimdanganya mke wako au mume wako sawa na kujidanganya wewe mwenyewe.
2. KUSIKILIZA USHAURI WA WENGINE NA KUTOA SIRI ZA NDANI
Kilichompatia nafasi Shetani (Nyoka) mpaka akampotosha Hawa, ni baada ya Hawa kuelezea sehemu ya udhaifu wake. "Mwanamke akamwambia nyoka, Mtunda ya miti ya bustanini twaweza kula: Lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale wala msiyaguse, msije mkafa"
Kosa la Hawa ni baada ya kuanza kusema "LAKINI", pale ndipo Nyoka akatambua wapi anaweza akawateka na akaelewa kumbe hiki ndicho walichokatazwa sasa ili nivunje uaminifu wao mbele za Mungu, nami ntawaambia wafanye hiki walichokatazwa.
Shetani siku zote huwa anatafuta kuzijua njia zetu na udhaifu wetu ili aweze kutunasa 2Kor 2:11 Shetani asije akapata kutushinda: kwa maana hatukosi kuzijua fikra zetu"
Kwa kuongea kwako ndiko kunakokutambulisha jinsi ulivyo ndani ya moyo wako Mathayo 12:34, Hivyo ni rahisi sana adui kukuangamiza.
Wanandoa wengi sana wanajikuta na wakati mgumu kwa sababu ya kushirikisha watu wengi sana katika matatizo na makwazo waliyonayo ndani ya nyumba (ndoa) zao.
- Tambua hili, si wote mnaowashirikisha kwamba wanaipenda ndoa yenu idumu.
- kadri unavyoshirikisha watu huwa Shetani ndipo anapojitahidi sana kuendelea kuwaharibu na kuwawekea mkandamizo ndani yenu.
- kutatua ninyi wenyewe tatizo ndani ya ndoa kunaupendo mkubwa unoongezeka katikati yenu kuliko ule eurejesho unaorejeshwa na viongozi wenu wa kiroho au wazazi au majirani n.k.
3. KUTOKUTAMBUA KOSA NA KUJUTIA KOSA.
Jambo gumu sana kwa mwanadamu yeyote ni hali ya yeye kuwa na moyo mgumu kutambua kwamba amefanya kosa. Hii ni dhambia namba 1 inayoambatana na dhambi ya kutokuamini. ni rahisi mtu kutubu na kutorudia kufanya kosa endapo umetambua kosa lako au udhaifu wako.
Kilichotokea Kwa Adamu na Hawa mpaka amesababisha kizazi chote cha mwanadamu kutokuwa na moyo wa kutubu na kutorudia kosa ni wao kutokutubu. hawakuingia kwenye kutubu kwa sababu kila mmoja alijiona hana kosa bali mwenzake anakosa.

"Akasema, ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza uyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. BWANA Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala."
Adamu anamsingizia mkewe Hawa, naye Hawa anamsingizia Nyoka, Mpaka Mungu anatoa adhabu hawa watu walikuwa hawajatubu kabisa.
nimeangalia ndoa nyingi sana kinachowafanya wahindwe kuelewana ni kutokujishusha mmoja wao, kila mmoja anaona akijishusha ataonekana anamakosa hivyo hawataki kuonekana wanamakosa hivyo wanazidi kugombana, kutukanana, na kushitakiana.
4. KUTOKUWA NA HOFU YA MUNGU, BALI HOFU YA ADHABU.
Wengi sana kwenye ndoa wanahofu na ahadi waliyowekeana kanisani au sehemu yoyote ile, maana ile ahadi ina adhabu nyingi ikiwemo fedheha kwa jamii, wazazi, ndugu n.k. Pia na adhabu ya kutengwa kanisani. Adamu hakuwa na Hofu ya Mungu kwani aliambiwa akila tunda la ule mti aliokatazwa hakika atakufa. kumbuka, aliyekuwa wa kwanza kula tunda alikuwa ni Hawa halafu badaye ndipo akampelekea mumewe ili ale, na Adamu alisisitizwa sana na Mungu kutokula lile tunda la ule mti, kilichomfanya Adamu akala ni kwa sababu aliona Hawa amekula na hajafa hivyo akaona kwamba Mungu alikuwa anamtania akaamua kula na yeye.
5. KUTOKUJUA NAFASI NA WAJIBU WETU KATIKA NDOA ZETU
Biblia inasema,
"Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha kila mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu" 1Kor 11:3
Adamu ndiye aliyekuwa wa kwanza kupewa maelekezo ya kutokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. kosa la Adamu akiwa kama kichwa cha mwanamke, baada ya mkewe kumpelekea lile tunda ili ale hakuchukua hatua za kumuuliza Mungu juu ya kukubali ushauri wa mke wake, akafanya uamuzi yeye binafsi pasipo kumuuliza Mungu je ni kweli umeamua kusema na Hawa tuanze kula haya matunda au?
nafasi ya Hawa, hakuchukua uamuzi wa kumshirikisha Adamu kabla hata ya yeye kula lile tunda, pia amgejaribu kumwita Adamu wakati nyoka bado yupo kwenye yale mazingira kama ilvyokuwa kwa Manoa (Baba yake Samsoni) pamoja na mkewe akiwa na yule Malaika.
Ni vizuri kujua wajibu wako mwanaume na wajibu wako kama mwanamke katika ndoa.
6. KUTOKUHESABU GHARAMA
Kunagharama katika kila jambo unaloliendea kulifanya,Unajua nyoka hakumdanganya Hawa bali alimwambia ukweli pasipo kumwambia gharama zake. Nyoka alisema:-

"Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya" Mwanzo 3:4-5
"BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya: na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala akaishi milele, kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi........" Mwanzo 3:22-24.
Nataka ujue kwamba Nyoka alisema ukweli ila hakumwambia gharama zake baada ya kujua mema na mabaya kwamba je! atamudu kuyatenda mema bila mabaya? sawa sawa na binti au mvulana aliyekuwa bikra halafu akaja kuyajua mambo hayo huwa asilimia kubwa wanashindwa kuhimili hali zao mtaa mzima utapata habari zake yeye tu.
- Mbinu ambazo mtu anaweza kukupa/kukushauri namna ya kutatua na kuimarisha upendo wako kwa mwenzi wako katika ndoa ni lazima uupime kwanza usije ukaleta matatizo badala ya kutatua matatizo, Hawa aliliona tunda la kupendeza sana na ili amfurahishe zaidi mume wake akaamua kumpelekea ili naye ale kumbe analeta balaa ndani ya ndoa.
7. KUTOTIMIZA KUSUDI LA MUNGU
Adamu ndiye aliyesababisha mpaka mkewe akaingia kwenye kushawishiwa na Ibilisi (Nyoka). Adamu hakumjengea imani iliyo sahihi Hawa itakayomfanya asimame kwenye msimamo wa kutokukubali ushauri wa nyoka katika kulila lile tunda. Imani huja kwa kusikia, inamaana Hawa hakuwa na imani iliyothabiti kwa sababu hakusikia ipasavyo kutoka kwa Adamu, na Adamu hakuhakikisha vizuri kwamba je huyu Hawa hata nikiwa mbali naye ataweza kusimama katika kile nilichomfundisha?
Mungu anamfanya mwanaume aone njia na mwanamke yupo pale kuangalia hatari kwenye njia, sasa endapo mwanamke hajajengewa msimamo uuliothabiti ndani yake kutegemeana na kile alichodhamiria mwanaume, ni rahisai sana Shetani kumtumia mwanamke kumfanya awe chambo katika safari.

Mwanaume anabeba maono ya kimaisha, na mwanamke anatakiwa abebe maono ya mwanaume, ajue hatari na aelewe kiuhalisia zaidi juu ya hayo maono, kusudi ajue namna ya kuyapeleka mbele na kutathmini wapi pamekwama. ndiyo maana shetani mara nyingi anatumia wanawake kuharibu kusudi la Mungu ndani ya mwanamume.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni