Daniel Gepson Mwasumbwe ni mwalimu wa Neno la Mungu, ambaye
amezaliwa Mkoa wa Mbeya wilaya ya Rungwe katika kata ya Itele. Alimaliza elimu
yake katika Shule ya Msingi Itele mwaka 2002 na kujiunga na elimu ya sekondari
ya Lufilyo mwaka 2003-2006. Kisha kujiunga katika Chuo Kikuu cha Kampala
International tawi la Dar Es salaam kwenye kitivo cha Technolojia ya Habari (Information Technology (IT)). Pia alichukua Masomo ya Bibilia katika
chuo cha Dr. K. A. Paul Dar es Salaam.
Na baadaye kufanya kazi sehemu mbalimbali kama mwalimu
akifundisha masomo ya Kompyuta katika shule mbalimbali za sekondari na vyuo hapa Tanzania. Hivi
sasa ni mwalimu wa Neno la Mungu ambaye anafundisha sehemu mbalimbali hapa
Tanzania ikiwemo Makongamano, semina za vijana, semina za wanandoa, pamoja na
masomo mbalimbali kibiblia.
Anamshuru sana Mungu kwa uaminifu wake, na kuachilia mzigo wa huduma ndani yake kwa namna ya ajabu mno. sifa, heshima, mamlaka na uweza vimrudie Yeye aliyeumba mbingu na nchi, Mungu wa Ibrahimu wa Isaka na wa Yakobo.
Anamshuru sana Mungu kwa uaminifu wake, na kuachilia mzigo wa huduma ndani yake kwa namna ya ajabu mno. sifa, heshima, mamlaka na uweza vimrudie Yeye aliyeumba mbingu na nchi, Mungu wa Ibrahimu wa Isaka na wa Yakobo.
Mwl D. Mwasumbwe
Ninamshukuru Mungu kipekee sana kwa jinsi ambavyo ameniita na akajifunua kwangu kwa namna ile ambavyo nimeweza kumtambua kwamba ni Mungu aliyeumba mbingu na nchi. nimeitwa na Mungu katika mazingira magumu na yenye changamoto sana kiasi ambacho ni rahisi kutokuendelea kufanya kazi yake, lakini Mungu ni mwema sana maana kufikia mpaka hapa ninamshangaa na kumshukuru Mungu sana. kuzaliwa kwangu na kukua kwangu kunamambo mengi yaliyokuwa yanajitokeza ambayo sikuweza kuyapambanua na kujua ni nini, lakini kwa kipindi hiki ndipo Muingu ananisemesha na kunielekeza sababu ya mambo yale kutokea ilikuwa ninini.
Nimezaliwa kwenye familia ya watoto saba (7) na mimi ni mtoto wa mwisho yaani wa SABA, wa kwanza kuzaliwa ni wakike na wanaofwata SITA wote ni wakiume, lakini Mungu akaniambia kwamba wazazi wako hawakupanga kuzaa watoto SABA, baali walipanga kuzaa watoto WANNE tu, yaani wakike wawili na wakiume wawili, lakini ilipotokea kufikia wa nne bado hajatokea wakike wakajaribu wa 5 wakaona ni wakiume, 6 naye wakaona ni wakiume, 7 wakaona ni wakiume (Ndiye mimi) walisema maneno mazito sana baada tu ya Mimi kuzaliwa na kuona ni mtoto wa kiume ambayo sitaweza kusema hapa. maneno hayo nilipoenda kuwaambia wazazi walishangaa sana na kuthibitisha kwamba ni kweli waliyasema hayo maneno baada tu ya mimi kuzaliwa. asante Mungu walisema maneno ambayo walikuwa wanamkabidhi Mungu maisha yangu yote ingawa wao walisema kuonesha kwamba wamechoka na hiyo hali, ingawa nimefika huku juu nimekabiliana na changamoto nyingi sana. nikamuuliza Mungu kwanini nilizaliwa mtoto wa saba na kwanini uliamua nizaliwe katika ile familia na nikawa mtoto wa mwisho, si hata tungekuwa wanne mi ungenifanya kuwa wa pili au watatu lakini ndani ya hiyo familia? Mungu alinipa sababu nyingi sana ambazo chache ntazisema lakini zingine ni za kifamilia na nyingine moja ni ya kwangu mimi binafsi.
Sababu ya kwanza: Mungu alinambia namba SABA (7) ni namba ambayo anaitumia yaani timilifu.
Sababu ya pili: alinipa Tito 1:3 "Akalifunua Neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu"
Mungu alisema, angeweza kunifanya nizaliwe wa nne lakini tambua wito wangu au Neno aliloachilia ndani yangu ni kwa ajili ya wakati kama huu au kizazi cha wakati huu. unapewa silabasi au somo fulani la kufundisha kutegemeana na darasa unalotakiwa kulifundisha, hivyo Mungu anapokuita hapa duniani ujue unakazi ambayo unatakiwa kuifanya kwa wakati kama huo na kwa muafaka. Mhubiri 3:1-3.
ningezaliwa mapema nadhani saizi ningekuwa mtu mzima na muda wa kumtumikia Mungu nisingekuwa nao mwingi sana.
Ninakumbuka mwaka 1996 niliumwa sana kiasi ambacho waliponipeleka Hospitali waliambiwa wazazi na madaktari kwamba "Mbona mmeleta mtu aliyekufa", Wazazi wangu waliomba na Mungu akamtumia Daktari mzungu sitamsahau jina aliita DR Zimma, akatumia vifaa vya Oxygeni kunihudumia kwa hali na mali mpaka Mungu akarudisha uhai wangu.
Ninakumbuka nilipona ajali ya gari iliyokuwa mbaya sana mnamo mwaka 2008 nilipokuwa ninafanya kazi kwenye gari za kaka yangu kama Kondakta. gari ilipata ajali ambapo namshukuru Mungu alimwambia dereva aniambie niiache gari iendelee kurudi nyuma maana ilishindwa kupanda mlima na nikawa naikimbilia ili niweke kidhibiti isimame, pale tu aliponiambia iache na nikaiacha nikaona inaanguka pembeni yangu. sitasahau siku hiyo kwani ilinisumbua sana akiili na saikolojia.
Nilipokuwa darasa la TANO wakati wa mchana wa saa TISA nilipokuwa nyumbani nikajisikia uchomvu wa ghafla ambao ulinipelekea kwenda kulala jambo ambalo lilikuwa siyo la kawaida kwangu. nilipokuwa nimelala ghafla nikachukuliwa kwenye maono na nikasikia SAUTI KUBWA MNO AMBAYO MAISHANI MWANGU SIJAWAHI KUSIKIA, hiyo sauti ni kubwa na ninaona dunia imefunguka juu na sioni hali ya mawingu wala chochote, ila hiyo sauti inasikika dunia nzima ikisema "NIMEKUJA KUCHUKUA ULIMWENGU". nilipoamka nikajikuta nimelowa jasho mwili mzima na nikaanza kuwatafuta wazazi walipo lakini ghafla sikuwaona nikaanza kulia kwani nakumbuka wakati mdogo nilikuwa napenda sana kutembea na mama kila mahali hivyo hata kwenye mikesha ya maombi, au semina au mikutano nilikuwa nakuwa karibu sana na mama jambo ambalo nililia sana kwani nilijua Mungu hataniacha na baba alikuwa na desturi ya kukaa chini ya mti akisoma Biblia lakini nilipotoka pale sikumwona nikakuta biblia na radio tu, lakini kumbe baba alikuwa kwa jirani na mama alikuwa kuchuma mboga. nilifurahi nilipowaona na nikawaambia yaliyonisibu walishangaa sana na baada ya hapo nakumbuka niliumwa lakini nikapona.
Huduma hii ya NEW POWER IN CHRIST (NPC) Mungu ameachilia ndani yangu rasmi 2012 nilipokuwa Mkoani Mwanza kikazi, na Mungu alinisemesha mambo mengi sana na kunijulisha ninini makusudi yake juu yangu. Mungu alinionesha wamama wengi na wabibi wakiwa wameshika fimbo kama mikongojo na pembeni yao wanazungukwa na watoto wengi sana, lakini nikauliza hii ni nini? ndipo nikaambiwa hawa ni WAJANE NA WATOTO YATIMA, hivyo nilisemeshwa Mengi sana ikiwemo na hivyo vitabu viwili KIJANA JITAMBUE NA ULIMWENGU WA SASA pamoja na MZAZI MLEE MTOTO NDANI YA KUSUDI LA MUNGU.
Huduma hii ina wahudumu zaidi ya 25 mikoa tofauti tofauti ikiwamo Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Morogoro, na Kilimanjaro. lakini tunaendelea kuomba Mungu aendelee kuinua watu sehemu zingine ambao watakuwa na mzigo na kazi ya Mungu katika kuitangaza Ijnjili ya Yesu Kristo.
Katika watu hao Tunawaimbaji binafsi na Timu, Tunawainjilisti ambao wapo WATATU, tuna wanamaombi pamoja na washauri.
Lengo la huduma hii ni kuhakikisha Tanzania Injili inahubiriwa na Neno la Mungu linafundishwa kiufasaha ili watu watoke kwenye vifungo vya uovu.
Mungu akubariki katika yote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni