MASOMO

MAMBO SABA (7) MUHIMU YA KUTAFAKARI NA KUZINGATIA WAKATI UNAFIKIRIA KUOA/KUOLEWA
Maisha ya ndoa ni maisha ya kipindi cha mwisho kwa Mwanadamu kilicho na mitihani mingi sana, kwani ni darasa tosha kwa wanandoa, na ndiyo maana katika uchumba unatakiwa upitie misukusuko kwani ni mojawapo ya mitihani ili ufikie kupata cheti wakati wa ndoa, na nikatafakari sana kwamba hapa duniani mwanadamu anapata cheti baada ya kufaulu mitihani, lakini kwa ndoa nikashangaa mtu anapewa cheti kwanza ndipo anapoingia kwenye mtihani wa maisha ya ndoa, sasa ni wewe kufaulu au kushindwa!

  1. Tambua unapoamua kuoa au kuolewa unakuwa unaunganisha familia tatu tofauti na zenye mifumo tofauti ya kimaisha.
Familia ya kwanza ni yenu nyie wawili yaani mke na mume, siyo rahisi kuweza kuishi kiraisi na mtu amabaye amelelewa kwao na mazingira tofauti na ya kwako, malezi tafauti kabisa, mawazo na mtazamo ni tafauti, mara ghafla mnaanza kuishi pamoja, na mnatakiwa kuwekana wazi kwa kila jambo na kufanya maamuzi yasiyoweza kuwafanya mgombane. Sasa katika nyie wawili mtegemee kujenga na kuzaa familia yenye mtazamo na taswira tofauti na familia zenu mlikotoka. Na familia zinazokuja hizi mbili ni upande wa mwanamke na upande wa mwanamume na kila familia ina tabia zake.
         Familia zingine badala ya baba kuwa kiongozi wa nyumba, utakuta mama ndiye kiongozi wa nyumba, inamaana kila analosema mama pale nyumbani ndilo linafwatwa, wala baba hawezi kuwa na maamuzi yoyote yale juu ya uamuzi atakaoufanya mama, sasa chukulia ndiyo unaoa msichana kwenye hiyo familia na ghafla anaanza kukuendesha na kuwa na sauti ndani ya nyumba kwa kila kitu, na kwa sababu alikotoka kwenye familia yao ameona mama ndiye kiongozi na mwenye sauti ya mwisho wa familia, na kwa sababu wewe mwanamume hayo mambo kwako ni mageni basi lazima muingie kwenye ugomvi.
         Umewahi kufikiri unaenda kuo/kuolewa kwenye familia ambayo ni wachawi! Vijana wengi kwa sababu ya tamaa zao wamejikuta wameishia kuoa/kuolewa na watu wachawi. Kuna kijana mmoja alikuwa ni mtumishi mzuri sana na Mungu alikuwa anamtumia vizuri sana lakini ilipofika kipindi cha kuoa akaaamua kuchagua binti fulani kanisani humohumo na huyo binti alikuwa anaonekana yupo safi kiroho na alikuwa mzuri hata wa sura, lakini watu walimshauri kwamba huyo binti hakufai na kwa huduma uliyonayo kwa kweli itakufa. Yule mtumishi hakuweza kuelewa ushauri wa wale watu, alin’gan’gana mpaka akamwoa yule binti na ilipofika kipindi wanapokuwa kwenye huduma vijijini pamoja na watumishi wengine, yule mtumishi akawa anashindwa kutumika kama hapo awali, mara Mungu akamfunulia mtumishi mwenzake, usiku akamwona yule mtumishi anakabwa na mke wake mpaka anaelekea kufa, ndipo wakatambua kwamba yule binti alikuwa siyo mzuri yaani alikuwa mchawi, basi mpaka sasa yule mtumishi anaishia kuwa kama waumini wengine kanisani kwani huduma ndiyo imekwisha kabisa mpaka sasa.
        Familia zingine huwa ni wachafu sana, yaani siku ukaenda nyumbani kwao ghafla bila taarifa, utashanga takataka mpaka mlangoni na mara nyingine hata kupiga deki ndani ni shida tupu, sasa unajiuliza humu ndani naingia nivue viatu au? Maana nikivua ni lazima nitachafuka na nisipovua watasema hana adabu. Sasa umewahi kufikiria ndiyo mwanamke anakuja unamwoa utashaagaa hata kitanda kutandika ni shida, nguo zinakaa mpaka sebuleni. na wanaume, siku mke kasafiri utajua tu kwamba leo mke wa fulani kasafiri, utashangaa kuona sebuleni pako ovyo, vitambaa ni balaa tupu utasema kunawatoto walikuwa wanacheza na kama alikuwa anajipikia basi utavikuta vyombo vimejazana na vinazungukwa na nzi, sufuria zina masizi mpaka ndani sasa sijui yaliingiaje mi sijui! Ni aibu hiyo jamani!, sasa hali ikiwa kama hivyo itapelekea magonjwa yasiyoeleweka. Badala ya kuona raha ya ndoa sasa unaanza kuona karaha ya ndoa kisa hukufanya uchunguzi na kufikiria kabla hujafanya maamuzi.
       Watu wengine ni wavivu sana, maandiko yasema “asiyefanya kazi na asile”, kunafamilia zingine jamani ni tabu tupu, ukiangalia wanapenda kuvaa vizuri sana na kujipenda sana na kanisani wanaenda sana, lakini ukiuliza wapi wanashamba la kulima watakwambia hamna. Kweli wengine wanaishi mjini mashamba ambapo hamna lakini nina maana hata sehemu ya kujipatia riziki angalau kidogo, wengine hata kujishughulisha na shughuli ndogondogo tu huwa hawawezi, hasa vijana wa kiume utashanga kuanzia asubuhi mpka jioni anaangalia Vidio (Television Vidio (TV)) na hapo anamchumba na anapanga kuoa, hata godoro hana na bado anakaa kwa wazazi wake, yeye huwa anasubiri asubuhi ifike anywe chai aliyopika mama au dada ndipo aende kijiweni na ikifika mchana atarudi kula chakula cha mchana na kurudi tena kijiweni, hivyohivyo na jioni na kama ndiyo siku ya ibada ndipo ataoga na kuomba sadaka kwa mzazi halafu aende kanisani. Mhh Mungu atusaidie sana.
       Familia zingine zinamazindiko sana, kwamba kila atakaye mwoa huyu binti wa kwanza ni lazima afe, au wanamwapisha kwamba huyu binti atakuwa anaishia kuwa mjane, pia hata upande wa mwanamume huwa mazindiko yapo, kwamba huyu kijana kila akioa hatakuwa anapata watoto. Nilipigiwa simu siku moja na binti, akaniambia nimwombee kwani alinenewa na shangazi yake ya kwamba hatakuja kupata mume wala mafanikio yoyote katika maisha yake yote, na hapo alipo alikuwa amewahi chumbiwa mara tatu na anaishia kuachwa pasipo na sababu, na sasa anaishia tu kukaka kwa dada yake, usije kushangaa hata mwenyewe unajaribu kupanga kuoa/kuolewa kumbe umefungwa lakini yote ni ushirikina wa kifamilia au huo ukoo.
       Pia kuna familia zingine au makabila mengine huwa wanadai mtoto wa kwanza kuzaliwa ili atolewe kama kafara, na usipoelewa hili litakugharimu pindi tu utakapokuja kumpoteza huyo mtoto na ndipo utakapoelewa, na ndiyo maana tunasema kijana kaa vizuri na Mungu naye atakupa macho ya rohoni utaona wapi panafaa kuoa/kuolewa. Kumbuka pia magonjwa mengine ya kurithi huwa yanafwatilia watoto wa kwanza kama vile kuugua kichaa, kifafa, kifua kikuu, UKIMWI n.k na hizo zinakuwa ni roho tu zinazofuatilia familia. Kumbuka unapounganisha mambo yote ya familia ya upande huu na upande mwingine unategemea utapata nini hapo?

  1. Unapoamua kuoa/kuolewa utambue unaenda kuwajibika zaidi
Kumbuka ya kwamba unapoamua kuoa/kuolewa unaenda kuanza maisha ya kipekee kwani hiyo ndiyo ngazi ya maisha yako ya mwisho mpaka kufa kwako, kumbuka siku utaitwa baba/mama mpaka utakuja itwa bibi/babu, kama Mungu atakujalia maisha marefu, hivyo kumbuka utakuwa umekusanya ndugu wa pande mbili zote, sasa usije sema mi naweza nikamlea mke wangu tu! Hapana, kumbuka kuna ndugu wa upande wa mke/mume wako watahitaji msaada je utaweza kumudu? Na maandiko yanasema;
“Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini” (1Timotheo 5:8)
Ni aibu na ni dhambi, pale unaposhindwa kuwahudumia ndugu zako wa nyumbani mwako, kumbuka kunamaradhi, kuna misiba, kuna wengine wanasoma kama mdogo mtu au kaka mtu hao watahitaji matumizi ya shule au ada, kuna mambo ambayo ulipokuwa peke yako uliona ni rahisi kufanya lakini pindi unapokuwa na ndoa unatakiwa kuwajibika zaidi.
       Mara nyingine kwa kijana wa kiume unaoa msichana ambaye ni wa kwanza kwao au ni tegemeo kwenye familia yao, na pindi unapoamua kumwoa inamaana tegemeo lote linakuwa ni wewe, sasa sikwambii usimwoe! Hapana, baali hakikisha umejipanga vizuri kukabiliana na majukumu aliyokuwa nayo kwao kwani huwezi kuwatupa ndugu wa upande wake, na siku nyingine watapenda kuja kukutembelea kwako, na wengine watapenda kulala kama ni mbali kidogo, sasa itategemea umejenga nyumba au umepanga nyumba ya namna gani, nasema hivi kwani nimeona pindi tu wanandoa wanapoingia wakiwa hawana hata muda mrefu huwa inaanza misuguano na ukifwatilia utakuta ni ndugu wanajaa nyumbani. Sasa jiandae unaeingia kwenye ndoa kubeba ugeni na kuwajibika kwa hali na maali.
        Kumbuka kunakuwajibika kimawazo pia, muda mwingine kunakuwepo na vikao mbalimbali vya familia ya upande wa mwenzi wako, nawe kama mwanafamilia unatakiwa kuwa na upeo wa kuweza kuchangia hoja na mawazo ya kimsingi, utashangaa shemeji mtu kwenye kikao anakuja ananuka pombe na anayoyafanya pale kwenye kikao mwenyewe mwenzi wake utatamani uzimie. Sasa kama yeye mwenyewe anashindwa kujilekebisha ataweza kweli kumpa mtu mawazo ya kumjenga? Na ndiyo hao wanafika kipindi wanatembea na wafanya kazi wao wa ndani na inayopelekea mpaka ndoa kuyumba.
        Hasa kwa mabinti nataka mnisikilize, ni aibu sana binti unaeingia kwenye ndoa halafu hujui kupika, unapika wali jinsi unavyoukologa loh! Utazani unakologa uji, na ukipika ugali unaekula utatakiwa uwe na maji ya moto pembeni kwani lazima ukutane na mabonge ya unga katikati ya ugali, sasa ni aibu na ndiyo maana wanaume wanaamua kula huko nje ndipo wanarudi nyumbani. Pia wanaume nanyi mnashangaza sana wengine hata kusonga ugali ni shida sana, na pindi mke anumwa wewe unaamua kununua chipsi, sasa sijui mtakulahizo chipsi mpaka lini, siku umeingia jikoni unaipua ugali mbichi kabisa. Nakumbuka nilitembelewa na rafiki yangu mmoja na mimi nilikuwa sishindi nyumbani, na pale nyumbani kuna kila kitu cha kuweza kupika, siku nimetoka kazini narudi nyumbani nikakuta hajapika kitu, nilipomuuliza mbona hujapika? Na umekula nini? Akasema nilinunua chipsi, nami nikajua aliamu tu kununua chipsi pengine kwa sababu ya uchovu, sasa kesho yake nikamwabia twende sokoni ukaje na mboga kwani mimi sitarudi! Tulipofika sokoni nikanunu mboga na nilipomwambia aendelee kupika, akasema utakuja kupika mwenyewe kwani mimi sijui kupika! hah! Yaani nilishikwa na butwaa, na nikweli kabisa alikuwa hajui na alikuwa kijana amemaliza chuo kikuu.
       Sasa unielewe kwamba unapooa unaenda kuwa na mipaka, kwamba ni lazima ukawajibike tu na hiyo mipaka ni ya baadhi ya mambo mengine kutokuyafanya, kama vile kurudi usiku nyumbani, kama ulikuwa unakesha kuangalia mpira kwa jirani yako sasa itabidi hiyo tabia ife, kwani siku utarudi utakuta mwana si wako.
        Kama bado hujaoa, weka mpangilio ni lini unaoa kusudi upangilie mipango na namna gani utaweza kukabiriana na majukumu, shida ipo sana kwa vijana wakiona fulani kaoa basi utashangaa naye huyu anakimbilia kuoa, we unajua mwenzio alivyojipanga? Weka malengo ndani ya muda fulani utakuwa umefanya mambo kadhaa ndipo uingine kwenye ndoa.
“Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”
 (Mhubiri 3:1)
Ujue kila kipindi unachopitia kuna takiwa uchukue hatua za mabadiliko kutegemeana na majira, na kama unajipanga kuoa baada ya miaka miwili inamaana kunamambo utatakiwa kuyafanya hapa katikati ili kujiandaa kukabiriana na majukumu ya ndoa. Pia kwa kadri tathmini utakavyokuwa unaiona ni rahisi kuwa na taswira nzima ya ndoa yako na kujua watoto utakao kuja kuzaa. Kunawengine wanaingia kwenye ndoa hata hawaelewi watazaa watoto wangapi na wengine hata wakati wa uchumba huwa hawajadili kwamba waje wazae watoto wangapi, sasa inapotokea mmeingia tayari kwenye ndoa na mwenzio anataka watoto sita na wewe unataka wawili sasa sijui mtakata rufaa wapi, mimi sijui! Zaidi mtakuwa mnaleta kuvutana kwenye suala la idadi ya watoto kila siku.

        Unapoamu kuoa angalia kwanza wewe ni tegemeo kwenye familia au lah! Unawadogo zako wanatakiwa kwenda shule na bado hawajaenda au ndiyo wapo shule, elewa unapoingia kuoa kabla ya hao watoto kuwawekea msingi mzuri ukitegemea kwamba ukioa utawasomesha, uwe na uhakika kabisa watayumba kwani maamuzi yako ya kuwasomesha ukiwa kwenye ndoa ni lazima umshirikishe mke wako, na siyo rahisi kukubali kila mwisho wa mwezi mshahara uende nyumbani kusaidia ada ya wadogo zako, na mara nyingi familia zimekwama kielimu na maendeleo mengine kwa sababu tu kaka aliyekuwa mwenye uwezo kaoa na baada ya kuoa akasahau kusaidia wazazi na wadogo zake.

  1. Itaendelea.........................................
Masomo mengine: -


1 Tambua madhara ya NGUVU YA AGANO KWENYE MAHUSIANO NA NAMNA YA KUTOKA ILI UFANIKIWE.

  
     2 ZIFAHAMU CHANGAMOTO KATIKA MAHUSIANO YA UCHUMBA NA NAMNA YA KUZIKABILI.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni