MALEZI YA KIKRISTO KWA MTOTO


            Unaweza ukawaza sana na kufikiri vile unavyoweza juu ya uzao wako, endapo unatambua wajibu wa wewe kuwa na familia. lakini hakuna kitu kigumu sana kama kuweza kulea mtoto katika maadili ya kumpendeza Mungu na jamii pia, hususani katika kizazi cha sasa ambacho asilimia kubwa ni vijana ambao Shetani amewakamata. 
            Wazazi wengi wameshindwa kupanda mbegu ya Mungu ndani ya watoto wao, siyo kwamba hawapendi, ila tu ni kwasababu ya kukosa uelewa namna ya kwasaidia watoto, pia kukosa muda wa kukaa na watoto kwa sababu ya shughuli za kimaisha, lakini Familia ni mojawapo ya majukumu yako ya kila siku ya kimaisha.

Njia za kuzingatia katika kulea mtoto tangu anapozaliwa.
1. Tenga muda wa Ibada nyumbani kwako na watoto wako.
2. Kila mtoto anapozaliwa tu! mnunulie Biblia, na kumpa maelekezo kwamba mwongozo wa maisha    yake yamo ndani ya Biblia.
3. Mpe muda wa nini anataka ajue, (maswali) kusudi ujue namna alivyo mdhaifu.
4. Jifunze kushiriki chakula kwa pamoja wote, utajua kirahisi tabia za watoto.
5. Usijaribu kumfokea mtoto mbele za watu. utamfanya awe anakuwa na hasira nyingi na kukosa           adabu anapokuwa mbele za watu.
6. Usimwadhibu nje ya eneo/wakati/ akiwa amekosea. kama kafanya kosa, utatakiwa kumwadhibu muda huo huo na eneo hilo hilo, kusudi ajue adhabu imetolewa kwa kosa la aina fulani, ili siku nyingine asirudie.
7. Jua anachokipenda, na umpe nafasi ya kile anachopenda kukifanya kama ni mbunifu (Creative), uelewe namna ya kumpa nafasi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni