Bwana wetu Yesu Kristo alisema "Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni" Yohana 17:18
"......Kama Baba alivyonipeleka mimi, mimi nami nawapeleka ninyi" Yohana 20:21b
Mpango wa Mungu kumtuma Yesu Kristo ni ili aje kuokoa kila roho iliyopote, na kufundisha habari za ufalme wa Mungu. Madhumuni ya Yesu Kristo kukuokoa wewe na si tu ili uende mbinguni, bali uweze kufanyika kama Yeye katika kuwafanya wengine wamjue Kristo Yesu na ndiyo maana ukiokoa tu huendi mbinguni bali unabaki hapa duniani ii uendelee kuwafanya wengine waokoke.
Wengi sana wanaokoka tu na kubaki jinsi walivyo pasipo kumzalia matunda Yesu Kristo kama vile alivyo tutuma, siyo kwamba wanapenda, bali ni kwa sababu hawajui kwamba mahali walipo kwa wakati huu hapastahili wao kuwapo, hivyo hawana msukumo ndani yao wa kutafuta kutoka.
Ili uweze kufikia Kiwango cha kumzalia Yesu Kristo matunda (Utumishi katika Kristo) kuna hatua kama nne (4)
Warumi 8:29-30
"Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagu tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita: na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza"
1. Kuchaguliwa
Ukisoma vizuri mistari hiyo ya Warumi utagundua hatua hizo nne. katika hatua ya kwanza ambayo Mungu anamchagua mtu kwanza tangu anapokuwa tumboni mwa mama yake (Yeremia 1:5), inamaana anakuwa anamjua kwa kazi yake maalumu.
Ndiyo maana maranyingi sana mtu anapata vita akiwa tangu tumboni mwa mama yake, kumbuka Esau na Yakobo jinsi ilivyokuwa. kila mtu anapokuja hapa duniani anakuwa amebeba kusudi la Mungu na mara nyingi sana Shetani huwa hapendi mwanadamu apate kujua kile alichoitiwa kwani atajikuta anang'ang'ana na Mungu.
2. Kuitwa (UTAMBULISHO WA WITO WAKO)
Suala la kuitwa huwa ni udhihirisho wa Karama ya Mungu katika maisha ya mwanadamu (Efeso 4:7-12) hasa katika Kristo Yesu. katika kuitwa huwa inatokea hali ya kusikia wito wa kutumika ndani ya moyo wa mtu. mara nyingi hatua hii mtu huwa anashindwa kushaulika katika utumishi, huenda kufanya kazi ya Mungu hata bila ya Mungu kumwambia aende, hujiona Yeye ni bora kuliko wengine katika utumishi (Shetani huwa ni rahisi kumteka).
Kawaida ya Mungu huwa anamwita mtu na kumpa maelekezo (Kumpaka mafuta) ndipo anamwambia sasa nenda, lakini wengi sana hatua hii huwa wanashindwa kuitumia ipasavyo, huwa wakisikia kuitwa tu huwa hawawezi kukaa magotini pa BWANA ili awape maelekezo ya kile alichowaitia, ndiyo utasikia Mtume na Nabii kumbe yeye ni mwinjilisti, utakuta anafungua kanisa kama mchungaji kumbe yeye ni mwinjilisti, matokeo yake baadaye huduma inakuwa ngumu na inaishia njiani.
3. Kuhesabiwa haki (Kuhakikishwa)
Suala la kuhesabiwa haki huwa ni hatua ambayo ni ngumu sana, Yesu kabla hajaanza huduma yake rasmi, alifunga siku 40 na baadaye akaingia kwenye majaribu ili kuthibitika, siku 40 zilikuwa ni siku za maandalizi ya mitihani na majaribu yale yalikuwa ni mitihani kwake. tunamwona Ibrahimu aliweza kuhesabiwa haki baada ya mtihani wa kumtoa mwanae wa pekee Isaka, na hakikuwa kitu rahisi sana kwa Ibrahimu.
- Wengi huwa wamekwama kwenye utumishi kwenye ngazi hii ya kuhesabiwa haki.
- Wengi watumishi hawapendi kuingia gharama katika kumtumikia Mungu
- Watumishi wengi huwa hawajui namna ya kutambua ya kwamba wapo kwenye hatua ya kuhesabiwa haki.
- Huwezi kuwa mwalimu wa mwingine pasipo wewe kuitia hilo darasa utakalofundisha mwingine (Ebr 5:12-14)
Unaweza kuhesabiwa haki kwenye mambo kama:-

- Kuwa na mfungo wa muda mrefu, kusoma neno pamoja na maombi.
- kutokuwa na pesa (Ugumu wa maisha) Unaweza ukaambiwa acha kazi ambayo ilikuwa inakuingizia kipato.
- Utii: Viongozi wako wa kiroho na wale wasio wa kiroho. Mdo 5:32, Rumi 13:1-3, Tito 3:1, 1Petro 2:13
4. Kuwatukuza.
Mungu anakuwa na uhalali wa kukutumia kwa namna apendavyo yeye, baada ya wewe kukubali na kuingia gharama kwa ajili yake. wengi waliopitishwa mahali pagumu sana baadaye wakaja kutukuzwa kama Ayubu, Ibrahimu, n.k
Unapewa upako wa kwenda kuwasaidia wengine upande wa kufundisha, kuhubiri, kutoa unabii, kuanzisha makanisa na kadharik. lakini pasipo kuwa na historia nzito huwezi kuwa na msukumo ndani yako wa kumshukuru Mungu na kumtukuza kwa ngazi aliyokupeleka nyingine. na hapo ndipo kila atakayekuona jinsi ulivyo kwa kweli atasema Yesu Ni Bwana!

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni