TAMBUA KUSUDI LA
NDOA NA NAFASI YA MWANAMKE KATIKA NDOA
I) Ndoa kama taasisi ya Mungu.
Kwa
kijana anayejitambua mara nyingi unapofikia wakati kama huu wa kutafuta mwenzi,
kwake huwa ni kipindi ambacho ni kugumu sana, kwa sababu anajua anakokwenda
hivyo mke kama ndiye msaidizi lazima uumize akili, lakini kwa yule
asiyejitambua, huwa anaona bora kuoa yeyote yule ilimradi kampenda kwa
mwonekano wake na ndiyo hizo ndoa ambazo hazidumu sana.
Kosea nguo kuvaa, watakwelekeza
ubadilishe, kosea njia watakwelekeza na utarudi, kosea kununua kiatu pengine
unaweza ukabadilisha au ukauza na kununua kingine, lakini ukikosea
kuoa/kuolewa, kwakweli utakuwa umeharibu dira yako na kusudi la Mungu ndani
yako. Ndoa siyo kitu rahisi rahisi tu, kwa kipindi kifupi hiki ninapokuwa
kwenye huduma sehemu mbalimbali hapa Tanzania
huwa tunakutana na matatizo ya ndoa, hasa kwa ndoa za Kikristo ukifunga
umefunga, nimejifunza vitu vingi sana
mpaka nikaingia kwenye maombi nipate kujua kwanini Mungu amemua kutokutengana
pindi ndoa zinaposumbua? Kwanini mara nyingi ndoa zinasumbua?
i)
Elewa kusudi la ndoa kama
kijana
a)
Ndoa yawakilisha umoja kati ya washiriki watatu wa
utatu Mtakatifu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu). Kama
vile washiriki watatu wa Utatu Mtakatifu walivyo nafsi tofauti bali Mungu
mmoja, ndivyo Mume na mke ni tofauti bali wameunganishwa na kuwa mwili mmoja (Mwz
2:24).
b)
Ndoa ni mfano wa uhusiano wa Yesu na Kanisa lake (Efe
5:22-33)
a.
Mke na amtii mumewe kama
kanisa linavyomtii Kristo.
b.
Mume na ampende mkewe kama
Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa kwa ajili ya kanisa.
c.
Inamana wanandoa wanapaswa kuwa mfano wa uhusiano wa
Kriso na kanisa lake.
c)
Kutokana na kitabu cha Mwanzo na vitabu vingine utaona
makusudi ya ndoa yalivyojitokeza.
a.
Urafiki, “BWANA Mungu akasema, si
vema huyo mtu awe peke yake,
nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwz 2:18)
b.
Umoja, “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba
yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja” (Mwz
2:24), Kunatofauti kati ya Umoja na kuwa pamoja, umoja ina maana nia moja,
lengo moja, mawazo yasiyopingana n.k. ndoa nyingi wanakuwa pamoja lakini hawana
umoja, ni sawa na kwenye mkusanyiko kama msibani au harusini, kwa wale wanakuwa
pamoja lakini utashangaa hawana umoja, huyu akiambiwa hivi yeye anafanya vile,
mwingine anawaza ataondoka saa fulani kwenda kwake.
c.
Uzao, ‘….Mungu akawambia Zaeni
mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha;….”
(Mwz 1:28)
“Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni
mkaongezeke mkaijaze nchi” (Mwz 9:1).
d.
Starehe, “Akamwambia mwanamke,
Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto;
na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala” (Mwz 3:16),
“Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye siku zote
za maisha yako….” (Mhubiri 9:9)
e.
Ulinzi dhidi ya uasherati, “Lakini
ikiwa hawawezi kujizuia na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa” (1Kor
7:9)
II) Nafasi ya Mwanamke kwenye ndoa
Mwanamke kwenye ndoa
katambulishwa kama msaidizi wa mwanamume hivyo inamaana kwamba mwanamume hawezi
kujitosheleza yeye kama yeye ni mpaka kuwepo mwanamke kama msaidizi wake, na
anaposema “Msaidizi wa kufanana” inamaansha “wa kukubaliana, “Mwenzi” wa
mwanamume, mwenyekumkamilisha na kumsaidia, siyo kuwa mtumwa wake. Na hii
inamaanisha:
i)
Mwanaume anahitaji masaada ili kuijaza nchi na jukumu
la kuitiisha nchi.
ii)
“Msaidizi” ni cheo kikubwa na cha heshima sana .
a)
Mungu mwenyewe wakati mwingine huitwa “Msaidizi”,
“ Ee BWANA, usikie, unirehemu, BWANA, uwe msaidizi
wangu”, (Zaburi 30:10),
“……Bwana
atanitunza, Ndiwe msaidizi wangu na mwokozi wangu….” (Zaburi 40:17),
“
“Hata
twathubutu kusema Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu
atanitenda nini?” (Ebr 13:6),
Ukitafakari
vizuri katika mistari hiyo utatambua neno msaidi limetumika kumpa nafasi Mungu
anayojitokeza kwa ajili ya mwanadamu, hivyo ni kama
Mwanadamu hawezi kufanya jambo bila huyu msaidizi Mungu.
b)
Roho Mtakatifu katumika kama
“Msaidizi” wetu,
“Nami nimemwomba Baba, naye atawapa Msaidizi
mwingine, ili akae nanyi hata milele, ndiye Roho wa kweli…” (Yoh
14:16,17),
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye
Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote
niliyowaambia” (Yoh 14:26),
Bwana Yesu Asifiwe! Endelea kusoma na (Yoh 15:26; 16:7)
.
Sasa kama hiki
cheo cha “Msaidizi ni chakumstahili muumba wa ulimwengu, basi inamaana hata
mwanamke anahadhi kubwa ya yeye kuwa “Msaidizi” wa mwanamume na hivyo mke
inabidi ajivunie kwa kuwa nacho hicho cheo, na kama ulikuwa hujui wewe mwanaume
kwa kumdharau mke wako nakushauri umpigie na magoti ukamwombe msamaha endapo
ulikuwa unamdharau.
Itanendelea ...............................................
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni