MADHARA YA ZAWADI KWENYE MAHUSIANO/UCHUMBA

Zawadi ni kitu chochote kile unachopewa/kutoa pasipo kugharamia wala masharti kwa mpokeaji/mtoaji.
     Nilikuwa nikitafakari mistari hii sana inayosema hivi:-
"Ataminiye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi" Mithali 15:27)
Nilitafakari sana juu ya zawadi na nikawaza sana kwa sababu watu wengi sana tunapenda zawadi na hakuna ambaye hajawahi kupewa zawadi wala kutoa.
     - Lakini tunaambiwa tusipozipenda zawadi ndiyo tutapata kuishi, ina maana kunamadhara ndani ya zawadi ambayo yanapelekea mtu kutokuishi.

Kadri nilivyoendelea kutafakari, Roho Mtakatifu akaanza kunisemesha na kunipa baadhi ya mistari na maelekezo yake, ambapo nikajua madhara kwa jinsia moja na madhara kari ya jinsia mbili tofauti yaaani mwanamke na mwanaume hasa walio wachumba au wanaofikiria.

Kwa jinsia Moja
(Mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke) Madhara yake.
" Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake" (1Samweli 18:1-4)
Nataka uone mambo kama manne yaliyopo hapa.
- Yonathani alikuwa ni mtoto wa mfalme Sauli.
- Sauli baada ya kumkosea Mungu, Mungu akaamua kumwondoa kwenye kiti cha ufalme.
- Ufalme wakati huo ulikuwa ni wakurithishana, yaani mtoto wa mfalme ndiye anayetakiwa kuchukua nafasi ya baba yake, hivyo mtoto anarithishwa ufalme.
-  Sasa aliyetakiwa kuchukua ufalme baada ya Sauli, ilimpasa Yonathani mwanae na Sauli aweze kuwa mfalme wa Israeli kwenye nafasi ya babaye.

Mungu alimkusudia Daudi chukue nafasi ya Sauli, hivyo mwenye kukabidhi na kuridhia atakuwa ni mtoto wa Sauli yaani Yonathani. Ndiyo maana Yonathani aliingiwa na roho ya kumpenda sana Daudi kwani alitakiwa kumkabidhi ufalme uliomhusu yeye Yonathani kutoka kwa baba yake. na ishara yake ilikuwa ni kumpa joho,

NB: Zawadi inaweza ikakuingiza kwenye agano kwa kutokujua au kwa kujua, inategemeana na mpokeaji au mtoaji wa hiyozawadi.
Mfano, unaweza ukatoa zawadi kumpa mtu kwa moyo mweupe lakini yule mtu akanuisha na kuifanya anavyotaka yeye ilimradi ilete madhara kwako.
           Pia mtu anaweza akainenea na kuinuiasha maneno anayojua yeye ilimradi ilete madhara kwa mpokeaji.
       
HIVYO SASA.

  • -Katika zawadi mtu unaweza ukatoa nafasi uliyo nayo katika familia, kama ni mkondo wa baraka ukajikuta zinaenda kwa mtu mwingine, hasa tabia ya kuvaa nguo za marafiki usiowaju, kama mashuleni vile na kadharika.
  • - Katika zawadi kuna kuambukiziana tabia flani flani, ndiyo maana marafiki wananguvu sana ya kuweza kumpandikiza mtu tabia ambazo alikuwa hana, kwa sababu ya kupeana vitu pamoja na maneno katika vinywa vyao.
  • - Katika zawadi unaweza ukahamisha akili zako na maono yako yakaenda kwa mtu mwingine au yakapotelea hewani, ndiyo maana watoto wakihamia mkoa au mji mpya endapo kama walikuwa na akili sana darasani utashangaa wanabadilika kimtazamo, wanakuwa duni, ni kwa sababu wamekutana na marafiki wapya wakanyonya ufahamu wao kupitia vitu na maongezi yao.
ZAWADI KATIKA UCHUMBA
        Biblia inasema "Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako" Mt 6:21
Hazina ni kama pesa au chochote unachokiona kinathamani kwako hasahasa upande wa samani (vitu)
  • Hivyo unpompatia zawadi mchumba wako inamaana unaupeleka moyo wako kwake. au kama mnapeana zawadi inamaana mioyo yenu inakuwa inaambatanishwa. (Kumbuka anayetakiwa kuwaambatanisha ni Mungu pekee na si zawadi)
  • Na moyo wako ukiambatana kwa huyo mchumba wako uwe na uhakika Mungu hawezi kuingilia kati au kukusemesha endapo jambo lolote lile linatokea, maana wakati wa uchumba ni wakati wa mitihani, matazamio, inamaana lolote laweza tokea (Ndiyo maana mnapoingia kwenye ndoa mnapewa vyeti), sasa likitokea jambo baya na moyo wako upo kwake ujue hutaweza ambilika na hata ukiambiwa hutaweza kuelewa na kukubali kuachana naye.
  • Hupelekea kujeruhiwa kwa nafsi, kuna mwingine amependa mahali pasipopendeka, sasa siku zote anayependa huwa ndiye wa kwanza kutoa zawadi. sasa endapo umeshatoa zawadi nyingi sana na ukaja kuachwa ni lazima utapata jeraha ambalo haliponi kirahisi kwani tayari moyo wako ulikuwa umekwisha kuuambanisha na moyo wa aliyekuacha, hivyo nafsi yako inachanwa.
  • Inapelekea kushindwa kumpata aliye sahihi wa kuja kuishi naye! utakapoingia kwenye kumwomba Mungu ili akupe mtu mwingine (Mume/mke), mara nyingi unajikuta unaomba kwa kulalamika sana, pia utajikuta unamwomba Mungu amrudishe yule yule wa kwanza aliyekuacha kwani moyo wako anao yeye. pia utajikuta unamkubali yeyote yule ilimradi uolewe au umwoe tu lakini pasipo maridhio ya moyo wako.
  • Hupelekea mtu kujenga upendo wake katika zawadi na siyo ule upendo wa kiuhalisia. mtu atakupenda kwa sababu unampatia vitu flani flani na endapo unakosa pesa ya kumnunulia hivyo vitu huwa kunatokea na migogoro kati yenu. hivyo hutaweza kutambua upendo ulio wa dhati.
  • Hupelekea ndoa baadaye kuvunjika au migogoro isiyoisha, mwingine anaamua kuoana nawe ili kuepusha aibu kwani ulikuwa unapeleka zawadi nyumbani mpaka wazazi wamehusika sana kupokea hizo zawadi, pengine mpaka ndugu wa karibu wanamfahamu kwa utoaji wake huyo mtu. sasa ukiangalia wewe ndani ya moyo wako hujawa na amani naye, jambo ambalo ukijaribu kumkataa itapelekea wazazi kukukalisha na kukusema kwani wamekula vyake sana. pia na wewe kujihofia usalama kwani unaweza ukajikuta unaingia kwenye shida kubwa mpaka unatishiwa maisha yako.
  • Mungu huthibitisha uchumba wenu pale ambapo kila mtu moyo wake upokwake yeye binafsi. Biblia inasema "Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, KABLA HAWAJAKARIBIANA, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. naye Yusufu mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, aitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu" Mathayo 1:18-20
Ukisoma vizuri utagundua kwamba, Mungu alichukua nafasi ya kusema na Yusufu baada tu ya Yusufu kuchukua hatua ya kuwa mbali na Mariamu. kile kitendo kilimpatia Mungu nafasi ya kusema nao kwani alishatambua kwamba kumbe hawa watu mioyo yao haijaambatana kiasi kwamba hata nikisema nao watanielewa kirahi. fikiria kingekuwa ndiyo kipindi kama hiki, kitu gani kingetokea, kwanza ni ugomvi mkubwa, pili ni ngumu kuwakuta watu wawe karibu kama ilivyokuwa kwa Yusufu na Mariamu halafu hawajaingia kwenye dhambi ya uzinzi.
         Vijana wengi wameingia mpaka kwenye tendo la ndoa hata kabla ya ndoa halafu wanategemea baadaye Mungu atakuwa nao, na hata kama si wako utajikuta mnaoana tu kwani mmetanguliza kujiunganisha ninyi wenyewe kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni