UPAKO WA ROHO MTAKATIFU

 MAANA YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU


a. Ni nafsi na uwepo wa Roho Mtakatifu katika kutusaidia kuyatambua na kuwa na uwezo wa kuyatimiza makusudi au mapenzi ya Mungu yaliyo katika moyo wa Mungu, ili kumpendeza Mungu; kama Daudi na BWANA YESU KRISTO walivyoupendeza Moyo wa Mungu.

Utendaji kazi wa Mungu kiuhalisia katika Ishara, Ajabu (uponyaji) na miujiza (Jambo ambalo kwa akili za kibinadamu si rahisi kutendeka). yaani vile ambavyo karama zote 9 zinavyoweza kutenda kazi katika viwango ambavyo Mungu amevikusudia.
Mafuta yanasaidia kulainishia kitu ili kiwe laini, Kupaka, kutia mafuta ni ili kitu kifanye kazi kwa ulaini, kwa uhuru (bila misuguano), kufanya maeneno magumu kuwa laini, hulwta kupooza maumivu, zaidi sana husaidia kufungua kiungo kilichofungwa. hivyo mafuta ya Roho Mtakatifu yanafanya utendaji kazi za Mungu kuwa mwepesi na si kwa kutumia akili za kibinadamu,

Kwa mfano: kutokuona aibu unapokuwa kwenye maombi (Unaweza ukalia sana), kutokuwa na aibu unapokuwa unahudumu (Mwalimu, Mwinjilisti, Mchungaji n.k). watu wanatakiwa Kulowanishwa katika mafuta ya Roho Mtakatifu wakati wa ibada na hata wanapokuwa popote pale (waliochaguliwa na Kristo (Wakristo)) kwa kusudi la kutimiza kazi za Kristo alizoatuagiza kuzitenda kwa msaada wa Roho Mtakatifu aliye tuahidia na ambaye anatupaka mafuta kwa kuzitenda kazi zake Mungu.

Upako =Nguvu za Mungu+Uwepo(Maombi)+Neno+Ahadi+Utii+Unyenyekevu.

Katika Agano la Kale, hivi vifuatavyo vilitiwa mafuta.
Wafalme  = Nguvu
Kuhani     = Uwepo
Manabii    = Ahadi

Katika Agano Jipya (wakati uliopo) Upako wa Roho Mtakatifu upo juu ya kila mtu ambaye ameokoka, amebatizwa katika Roho Mtakatifu, akiwa amejitoa kikamilifu kwa Yesu Kristo katika kutuwezesha:-

  • Kutawala na kumiliki katika maisha kama wafalme.
  • kuwasilisha watu kwa Mungu na kuleta watu kwa Mungu kama Makuhani.
  • Kutoa Neno la Mungu mbele za watu katika viwango na uvumilivu kama wa Kristo.
  • Kuhubiri, Kufundisha, kushusha, kuabudu, kuomba na kuimba kama Manabii (Ufunuo 1:5-6)
Upako huvunja kila nira ya kifungo katika maisha yetu na kuweka huru kutokana na:-
  • Magonjwa, maradhi, mauti na hukumu.
  • Laana, mikandamizo ya mapepo na Uchawi
  • Tamaa ya mwili, dhambi na ulevi.
  • kazi zote za Shetani na kushindwa  (1Yoh 3:8)
  • Kutosamehe, kinyongo na hatia,n.k, kutokana na desturi mbalimbali za kidini (Isaya 10:27/ Matendo 10:38/ Zakaria 4:6)

 TABIA ZA MTU MWENYE UPAKO AU ALIYEJAA UPAKO!

i. KUITWA/ WOKOVU – kutambuliwa, kuitwa, kukubaliwa, kuteuliwa na Mungu; 
anakuwa ni mtu mwenye wito maalumu kwa kusudi maalumu la Mungu; hivyo 
kupata kibali mbele za Mungu na wanadamu(japo si wote), yaani, kumpendeza 
Mungu na wanadamu wenye mapenzi mema; anakuwa ni mtu mwenye kumpa 
Mungu utukufu wote, na wanadamu wanakuwa na amani nawe! Luka 2:52.

ii. WITO ni sauti isikikayo moyoni mwa mtu kwa:
1. Nia ya moyoni ya kumpendeza Mungu
2. Moyo wa kupenda, wa hiari, kupendezwa
3. Msukumo au mguso wa moyoni
4. Kukereketwa moyoni na kushindwa kutulia kwa ajili ya mambo ya Mungu.
5. Wivu wa moyoni kwa ajili ya mambo ya Mungu.
6. Kiu, njaa, na hamu ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu na utukufu wa Mungu tu!

iii. KUJAZWA AU KUPEWA NEEMA-Kuwezeshwa, kupewa nguvu, kutumiwa na Mungu na kupata ushindi au kufanikiwa (kuwa na uwezo maalumu) Warumi 8:31-39; Sababu:
1. Anatenda lililokusudiwa kwa kusudi na mapendi ya Mungu
2. Lililo kwa wakati wa Mungu
3. Mahali alipopakusudia Mungu
4. Kwa wakati alioukusudia Mungu
5. Kwa namna ile aitakayo au aliyoikudusia Mungu
6. Kwa nguvu zisizopingika za Mungu 
7. Lililo kwa uongozi wa Roho Mtakatifu – si kwa uwezo,wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho … Zekaria 4:6.

iv. KUTUMIKA – kuifanya kazi maalumu ya Mungu inayodhihirika kwa matokeo yake mazuri kwa Mungu, kanisa, na kwa watu wengine; Agizo maalumu. Huduma mbali mbali (Warumi 12:3-21) kwa mfano: kushuhudia, kuhubiri, kufundisha, umisheni, utoaji, maombi na maombezi, huduma kwa wasiojiweza…

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni