NAMNA AMBAVYO ROHO MTAKATIFU ANAWEZA KUKUPA NGUVU ZAKE KATIKA MAOMBI

Kunautofauti kati ya kuwa na Roho mtakatifu na kuwa na Nguvu za Roho Mtakatifu. Unaweza ukawa na Roho Mtakatifu lakini huna Nguvu za Roho Mtakatifu, ila siyo rahisi ukawa na Nguvu za Roho Mtakatifu pasipokuwa na Roho Mtakatifu.
  • Mtu anapookoka tu huwa anapokea Roho Mtakatifu ambaye anamsaidia katika kuhuisha tunda la Roho ndani ya mwamini.
      • Uvumilivu
      • Katika kushinda dhambi (dhamiri ya ndani humshuhudia dhambi)
      • Upole.
      • Upendo.
      • Furaha.
      • Amani. N.k
Hayo yote yanaundwa (yanatengenezwa) na Roho mtakatifu ndani ya mwamini.
Ukisoma Yohana 20:21 Biblia inasema
“Basi Yesu akawaambia tena, amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo akawavuvia, akasema, Pokeeni Roho Mtakatifu.”
Nataka uone vizuri neno hili “Akawavuvia……Pokeeni Roho Mtakatifu”. Hayo maneno Yesu aliyasema baada tu ya kufufuka, na kabla tu ya kupaa baada ya kukaa siku arobaini tangu afufuke aliwaambia wanafunzi wake maneno haya:-
“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” “Matendo ya Mitume 1:8
Angalia neno “Mtapokea nguvu”, kumbuka mara ya kwanza aliwavuvia Roho Mtakatifu na mara ya pili anawaagiza wasiondoke mjini mpaka pale watakapopokea NGUVU za Roho Mtakatifu.
  • Nguvu za Roho Mtakatifu huwa zinadhihirishwa kwenye utendaji na matokeo ya tendo. Ndiyo maana aliwaambia “wasitoke Yerusalemu, bali wangoje ahadi ya Baba”. Yesu alijua hawa wanafunzi ndiyo watakaoedeleza kazi zake hapa duniani hivyo hawawezi kutenda kazi zake bila kuwa na nguvu za Roho Mtakatifu.
Narudia tena “Roho Mtakatifu anakupa msaada na maelekezo binafsi namna ya kutembea ndani ya kusudi la Mungu, Lakini Nguvu zake zipo kwa ajili ya kufanya kazi zake katika maelekezo unayopewa na Roho Mtakatifu”
  • Huwezi kufanya kazi ya Mungu au kutimiza kusudi la Mungu pasipo Nguvu za Roho Mtakatifu,
Ukisoma Matendo ya Mitume 19:13
“Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni akina nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa”
Kilichowafanya wavamiwe hawa wana wa Skewa ni kwamba hawakuwa na mamlaka ya kulitumia Jina la Yesu Kristo, kwani hawakutambulika kwenye ulimwengu wa Roho kwamba ni wana wa Mungu, ndiyo maana waliambiwa “Yesu namjua na Paulo namfahamu lakini ninyi ni akina nani?”
“Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu”
Waefeso 1:13
Unapokuwa umeokoka unapigwa muhuri wa Roho Mtakatifu kukutambulisha kuwa mwana wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Hivyo kinachofwata baada ya kupigwa muhuri ni kutafuta kupokea nguvu za Roho Mtakatifu ambazo zitakuwezesha katika utendaji kazi za Mungu katika eneo alilokuweka. Sasa hawa wana wa Skewa hawakuwa na Nguvu za Roho Mtakatifu wala alama ya muhuri wa Roho Mtakatifu jambo ambalo likawapelekea kuvamiwa wao wenyewe na mapepo.
  • Usishangae mtu anamwombea mtu mwenye pepo au mgonjwa wala hafunguliwi, lakini mwingine akiombea mara moja tu anafunguliwa, utofauti ni kwamba mmoja hana nguvu za Roho Mtakatifu za kutosha ndani yake ambazo zitaweza kumfungua huyu mgonjwa, na huyu mwingine anazo za kutosah.
  • Nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya mtu zinakaa kama Chaji/umeme, pia zinaweza zikapungua kulingana na jinsi ulivyotumika.
“aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma akaligusa vazi lake, maana alisema Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona……..mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka katika mkutano, akisema, Ni nani aliyeligusa mavazi yangu?”
Marko 5:26;30
“Na makutano yote walikuwa wakitaka kumgusa, kwa sababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote”
Luka 6:19
“na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake”
(Efe 1:19)
Watumishi wanaelewa, ukishikana mikono au kusalimiana na mtu mwenye mapepo utashangaa unahisi kama mkono unauma. Ujue kunanguvu iliyoko ndani yako inapambana na nguvu iliyoko ndani ya mtu mwingine ambayo ni madhabahu tofauti na ya kwako.
Mungu anahitaji uombe kitu/jambo ambalo ni mpango/mapenzi ya kwake 1Yoh 5:14, hivyo ni rahisi sana Roho Mtakatifu kukupa nguvu na maelekezo katika jambo ambalo unatakiwa uliombee,lasivyo kama siyo mpango wa Mungu kuliombea utaona husikii nguvu wala msukumo, na si wengi sana huwa wanatambua na kujua kwamba jambo linalowazunguka linatakiwa kuombewa. Unaweza ukatazama jambo la kuliombea na usipoelewa kama ni la kuliombea linaweza likakuondolea imani yako Kwa Mungu au kukuvuruga kifikra na mfumo wako wa kimaisha kwani utakuwa unaona ni kero kwako.

- Nataka tuone namna ambavyo Roho mtakatifu anaweza kukupa nguvu zake katika maombi, na kwanini baadhi ya watu wanaombea jambo lakini ndani yao hawana msukumo wa kuliombea ingawa wanaona kwamba kunaumhimu wa kuliombea.
v     Kukaa kwenye eneo husika (ambalo Mungu amekuweka kama kuhani) na kuelewa Ishara/Viashiria vya Roho Mtakatifu anapokutaka uombe.
Kila mmoja (aliyeokoka) anafanyika kuwa kuhani/balozi/wakili/ 1Petro 2:5, 2Kor 5:20, 1Kor 4:1-2. kwenye ulimwengu war oho unapookoka Mungu anakuangalia wewe pamoja na watu wanaokuzunguka, kusudi aone kama je lile neno alilosema Kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi” je linatimizwa?
Kila mmoja anakazi yake maalumu kwenye ulimwengu wa roho, na Mungu anachotaka anahitaji ujue mambo yote yatakayotokea kwenye hilo eneo kabla yaw engine hawajayaona. Mungu ameweka mipango au picha kamili ya kila jambo kwenye ulimwengu wa roho juu ya mambo yanayokuzunguka, hivyo anahitaji watu wayajue hayo mambo kusudi yasipotokea wajue namna gani ya kuomba mpaka yanakuja kutokea.

Utajuaje kwamba Mungu anahitaji uombee jambo Fulani ambalo kalikusudia kwa wakati?




 Inaendelea

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni